WATAALAMU WANAKAGUA ITIFAKI KUHUSU WIZI WA NG’OMBE

Home/News/WATAALAMU WANAKAGUA ITIFAKI KUHUSU WIZI WA NG’OMBE

Tarehe 24 Februari 2021, kamati ya kisheria ya EAPCCO ilifanya warsha kupitia mtandaoni kujadili kuhusu itifaki ya Mifugo iliyotiwa sahihi mnamo 2008. Itifaki hii inahusu kuzuia, kupambana na kumaliza wizi wa ng’ombe Afrika Mashariki.

Warsha ilipangwa na ofisi ya EAPCCO na mradi wa ISS-Enact na ilihudhuriwa na wajumbe kutoka Comoro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan na Tanzania

Warsha hii ilileta mapendekezo kwa wakurugenzi wa upelelezi kuhusu mabadiliko yaliyopendekezwa kwa itifaki hiyo na walipendekeza mfumo thabiti wa kutekeleza utakaopitishwa na wakuu wa polisi.