Ujumbe Kutoka Kwa Kiongozi Wa Ofisi Ya Kikanda Na Mkuu Mtendaji Wa Ofisi Ya Eapcco

Home/press/Ujumbe Kutoka Kwa Kiongozi Wa Ofisi Ya Kikanda Na Mkuu Mtendaji Wa Ofisi Ya Eapcco

Nafurahia kuwakaribisha wageni wote katika tovuti ya Shirika la Ushirikiano wa Wakuu wa Polisi la Afrika Mashariki [Eastern Africa Police Chiefs Cooperation Organization (EAPCCO)]

EAPCCO ni shirika la kikanda la kutekeleza sheria lililo makini kuambatanisha huduma ya kitaifa ya polisi katika kikanda cha Afrika Mashariki na lenye lengo la kukabiliana na uhalifu wakupangwa wa kimataifa. Katika ulimwengu wetu wa utandawazi, ushirikiano wa polisi ni jambo la uhitaji na wala si la chaguo. Ijapokuwa katika ngazi ya ulimwengu, mashirika ya polisi yanashirikiana kupitia INTERPOL na katika ngazi ya bara kupitia AFRIPOL, kuna uhitaji mkubwa wa kutengeneza mifumo ya ushirikiano katika ngazi ya kikanda ili kushughulikia adhabu dhidi ya uhalifu wa kimataifa na hata pia uhalifu unaohusisha kuvuka mipaka ya kikanda pekee na hili ndilo jukumu linalotekelezwa na EAPCCO.

Kwa zaidi ya miongo miwili ya kuwepo kwake, EAPCCO imekuwa katika mstari wa mbele katika kukuza ushirikiano kati ya nchi ambazo ni wanachama kupitia usambazaji wa habari, maazimio ya wakuu wa polisi, mafunzo na operesheni za pamoja, huku ikilenga uhalifu wa kama vile ughaidi, ulanguzi wa dawa za kulevya, ueneaji wa silaha ndogo ndogo; uhalifu wa kimazingira; usafirishaji haramu wa binadamu na magendo ya binadamu; biashara ya vitu bandia; uhalifu wa mtandaoni na utapeli wa pesa na mwengineo. Shirika hili, kupitia baraza la wakuu wa polisi, kamati ya kuratibu ya kudumu na vitengo vyengine visaidizi (vya kimafunzo, kisheria, dhidi ya ughaidi na vya kijinsia) limeendelea kusaidia ushirikiano wa kikanda. Mafanikio haya hata hivyo yasingefikiwa bila ya usaidizi thabiti wa viongozi wa kisiasa na washirika wetu tunaowathamini.

Jukwaa hili la kidijitali ni kama njia ya kusambaza na kuonyesha mafanikio ya shughuli na mipango ya EAPCCO na pia kupata usaidizi wa umma katika mapambano dhidi ya uhalifu wa kimataifa wakupangwa.

Karibu!