Habari zinazotuhusu sisi

Shirika la Ushirikiano wa Wakuu wa Polisi la Afrika Mashariki [Eastern Africa Police Chiefs Cooperation Organization (EAPCCO)] ni shirika la polisi la kikanda ambalo wanachama wake ni Wakuu wa Polisi katika nchi 14. Lilianzishwa mnamo 1998 kwa lengo la kuoanisha, kuimarisha ushirikiano wa polisi na mikakati ya pamoja, kusambaza habari zinazohusiana na uhalifu na kuoanisha sheria ili kuongeza uwezo wa Mashirika ya Utekelezaji wa Sheria kupambana na uhalifu wa kimataifa.

office

Muundo wa EAPCCO unajumuisha Baraza la Wakuu wa Polisi [Council of Police Chiefs (CPC)] wa nchi hizo 14. CPC inasaidiwa na kushauriwa na Kamati ya Kuratibu ya Kudumu [Permanent Coordinating Committee (PCC)] inayojumuisha Wakuu wa Idara za Upelelezi wa Jinai wa nchi hizo. CPC iliunda kamati ndogo nne; Kamati Ndogo ya Jinsia [Gender Sub-Committee (GSC)], Kamati ndogo ya Sheria [Legal Sub-Committee (LSC)], Kamati Ndogo ya Mafunzo, na Kamati Ndogo ya Kukabiliana na Ugaidi. Kamati hizi ndogo zinawajibika kwa; kutunga mikakati, kuunda mifumo ya utendaji, na jukumu lengine lolote ambalo CPC inaweza kuwapa katika kupambana na uhalifu katika kikanda hicho. Ili kushughulikia mada yoyote hususa, CPC imeamriwa kuunda vitengo vya kazi vinavyojulikana kama Vikundi vya Kufanya kazi kutekeleza maagizo au kazi yoyote inapohitajika.

EAPCCO inafanya Mkutano wake Mkuu wa Mwaka ikizunguka katika nchi hizo ambazo ni wanachama. Ofisi ya KIkanda ya INTERPOL inafanya kazi kama ofisi ya usimamizi.

Lengo La EAPCCO
 1. Kuoanisha, kukuza, kuimarisha na kuendeleza ushirikiano na mikakati ya pamoja ya usimamizi wa aina zote za uhalifu unaovuka mipaka na unaohusiana na uhalifu wenye athari kwa kikanda
 2. Kuandaa na kusambaza habari muhimu juu ya vitendo vya uhalifu na kusaidiana kudhibiti uhalifu ndani ya kikanda kama itakavyohitajika kwa faida ya nchi zote ambazo ni wanachama.
 3. Chunguza mahitaji ya kimafunzo hususa kwa vikosi vya polisi vya wanachama, mafunzo ya kitaalamu kama vile kushughulikiamihadarati, magari ya wizi, vitu vya sanaa vya kuibiwa, uhalifu wa kiuchumi na kifedha, biashara haramu ya silaha, uhalifu wa vurugu pikijumuisha ugaidi na mashambulizi ya silaha, na maeneo mengine yoyote yanayoweza kutambuliwa.
 4. Identify training potential within the region for the benefit of member police forces/services and ensure efficient operation and management of criminal records and effective joint monitoring of cross border crime taking full advantage of the relevant facilities available through INTERPOL.
 5. Kuratibu mipango ya mafunzo.
 6. Kufuatilia utekelezaji wa, na kuzingatia kupitisha maazimio yote yaliyotolewa na EAPCCO.
 7. Kuoanisha vifungu vya kisheria vya nchi ambazo ni wanachama zinazohusiana na kukabidhi muhalifu kwa nchi inayopasa na usaidizi wa kisheria, na kutoa mapendekezo yanayofaa kwa serikali za nchi ambazo ni wanachama kuhusiana na hayo na mengineyo yanayoathiri ufanisi katika kudumisha sheria katika kikanda.
 8. Kuanzisha vitengo kama hivyo na kutengeza stakabadhi za kisheria kama itakavyohitajika ili kutekeleza madhumuni yake.
 9. Kutekeleza vitendo na mikakati yoyote muhimu na inayofaa kwa madhumuni ya kukuza ushirikiano wa polisi wa kikanda kama hali ya kikanda inavyoamuru.
 10. Kusaidia nchi ambazo ni wanachama kutengeneza au kuboresha vitendo vizuri katika utawala na usimamizi wa taasisi za polisi na kwa haki za binadamu.
 11. Assist member countries to develop and improve community based policing to encourage citizen involvement in preventing and combating crime.
 12. PKukuza ushirikiano katika upangaji, ukusanyaji, na panapofaa kuwatuma maafisa wa kutekeleza sheria na maafisa wa polisi katika shughuli za kuleta amani zinazoendeshwa na umoja wa Afrika.