Usafirishaji haramu wa binadamu
USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU NA MAGENDO YA WAHAMIAJI

Usafirishaji haramu wa binadamu unamaanisha usajili na usafirishaji haramu wa watu kwa njia ya nguvu, tishio, kulazimishwa, udanganyifu, au utekaji nyara kwa kusudi la dhulma. Ufafanuzi wa Kimataifa wa usafirishaji haramu wa binadamu uko katika Itifaki ya Palermo iliyopitishwa na U NGA huko Palermo, Italia mnamo Disemba 2000.

Usafirishaji haramu wa binadamu ni tishio ulimwenguni kote ambalo linagusa karibu kila sehemu ya ulimwengu. Karibu kila nchi ulimwenguni inaathiriwa na usafirishaji haramu, iwe ni nchi ya asili, mahala wanapopitia, au wanakoelekezwa/fikio la wahasiriwa.

Magendo ya wahamiaji kwa upande mwingine yanamaanisha ununuzi ili kupata faida

ya kifedha, kuingia kwa haramu kwa mtu katika nchi ambayo mtu huyo sio raia wa kitaifa au mkazi wa kudumu.

Tofauti kati ya usafirishaji haramu wa binadamu na magendo ya wahamiaji bado haiko wazi na uzoefu unaonyesha kuwa kuna visa vinavyoingiliana ambapo magendo yanakuwa usafirishaji haramu.

KUSAFIRISHA BINADAMU KIHARAMU KATIKA KIKANDA CHA AFRIKA MASHARIKI

Kikanda cha Afrika Mashariki ni mahali ambapo biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu inakua kwa haraka barani Afrika na inajumuisha nchi ya chanzo, yakupitisha binadamu, na nchi wanayoelekezwa/fikio. Mfumo na aina za usafirishaji haramu na magendo katika kikanda hiki kawaida huingiliana. Wahamiaji mwanzoni hutafuta msaada wa wasafirishaji wa kimagendo, lakini baadaye mara nyingi wanakabiliwa na usafirishaji haramu.

Mfumo huo umebadilika na kuwa uhalifu wakupangwa wa kimataifa unaohusisha mitandao ya jinai. Waathiriwa wengi wanasafirishwa ndani ya kikanda na sehemu kubwa inasafirishwa kwenda Ulaya, Mashariki ya Kati, au Afrika Kusini. Usafirishaji haramu wa ndani una hadhi ya chini ingawa umeenea katika nchi zote ambazo ni wanachama wa kikanda hiki. Usafirishaji haramu wa kindani haswa kwa wanawake na watoto kwa madhumuni ya kazi ya nyumbani, utumwa, kazi ya kulazimishwa, na ukahaba umekithiri.

Waathiriwa katika kikanda husajiliwa na mashirika halali au haramu au huhamia kwa hiari Kusini Mashariki mwa Asia na Asia ya Mashariki kutafuta ajira, ambapo wakati mwingine wanadhulumiwa katika utumwa wa nyumbani, biashara za kukanda, na madanguro, au kulazimishwa kwa kazi za mikono.

Familia zina jukumu kubwa katika kufadhili uhamiaji usio wa kawaida na zinaweza kulazimisha watoto wao kwenda ng’ambo au mijini kupata ajira.

MWITIKIO WA EAPCCO KUHUSU USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU NA MAGENDO YA WAHAMIAJI

Usafirishaji haramu wa binadamu ni moja ya uhalifu ulio na kipaumbele chini ya RB Nairobi na umetengewa sehemu ya kuratibu kupambana na shughuli za usafirishaji haramu wa binadamu katika kikanda hicho. Kwa kuongezea, Wakuu wa Polisi wa EAPCCO wanaangazia umuhimu mkubwa kwa shughuli zote za Kikanda zinazolenga kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu na magendo ya Wahamiaji na hii imeonyeshwa katika maazimio kadhaa yaliyopitishwa wakati wa mikutano mikuu ya kila mwaka ya EAPCCO. Kwa hivyo, EAPCCO inajitahidi kuwezesha mashirika ya utekelezaji wa sheria katika nchi ambazo ni wanachama wetu kushughulikia visa vya ulanguzi wa binadamu kupitia njia tofauti ikiwa ni pamoja na (ijapokuwa sio hizi pekee):

  • Kukuza uwezo wa mashirika ya utekelezaji wa sheria kuhakikisha kuwa maafisa wamewezeshwa kutambua na kuchunguza visa vya usafirishaji haramu wa binadamu wa aina zake zote, ikiwa ni pamoja na (ijapokuwa sio hizi pekee) kazi ya kulazimishwa, unyanyasaji wa kijinsia, vitendo vya uhalifu vya kulazimishwa, na kuondolewa kwa viungo.
  • Shughuli za ulinzi wa watoto na kufanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na vitengo vya ulinzi vya watoto na mashirika mengine yanayoshughulikiwa na ustawi wa watoto ili kuhakikisha uangalifu unaofaa unazingatiwa wakati wa uchunguzi unaohusisha uhalifu dhidi ya watoto.
  • Kupeana uwezo wa kutekeleza sheria na utaalam wa INTERPOL ambazo ni zana na huduma zinazowezesha kusambaza habari zinazohusiana na utekelezaji wa sheria kati ya nchi zote ambazo ni wanachama wa INTERPOL;
  • Kutoa msaada wa kiufundi na mwingine wowote kwa nchi ambazo ni wanachama katika kutekeleza shughuli zinazojumuisha ulimwengu wote ili kuvuruga na kusambaratisha mitandao ya usafirishaji haramu wa binadamu;
  • Uanzishaji wa ushirikiano unaohusisha kufanya kazi katika sekta zote ili kuboresha njia ambazo usafirishaji haramu unaweza kutambuliwa, kuripotiwa na kuchunguzwa. Kwa mfano, Ofisi ya Kikanda ya INTERPOL inashirikiana na Tume ya umoja wa Afrika katika utengenezaji unaoendelea wa kituo cha utendaji cha Kikanda [Regional operational center (ROCK)] kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu huko Khartoum Sudan.
  • Kuandaa na kuunga mkono hafla na mikutano ambayo inahusisha wataalam kutoka sehemu mbali mbali duniani;
  • Kushiriki katika vikundi vya wataalam vinavyolenga kazi za polisi zilizo mstari wa mbele na kubadilishana habari za utendaji.

Changamoto ya msingi inayotukabili sote katika kikanda hiki kama watu binafsi, mashirika ya kiserikali, mashirika ya kijamii, na mashirika ya kimataifa inabaki hivyo hivyo. Tunahitaji kuongeza mara mbili tena juhudi zetu za kuzuia usafirishaji haramu, kutambua na kulinda wahasiriwa na kuvuruga mitandao ya jinai inayofanya uhalifu huu, mwitiko wetu ukizingatia mabadiliko ya mbinu za usafirishaji haramu wa binadamu.