Uhalifu wa mtandaoni

Uhalifu wa mtandaoni ni uhalifu dhidi ya kompyuta na mifumo ya habari kwa lengo la ufikiaji na udhibiti wa kifaa bila idhini au kumnyima mtumiaji halali au mmiliki kufikia mfumo huo. Ukuaji wa uhalifu wa mtandaoni ni jambo la kushangaza na unakadiriwa kwamba dola bilioni 600 zilipotea mnamo 2018 tu. Hali tata ya uhalifu huu ni kwamba hufanyika katika eneo lisilo na mipaka la mtandao na inachangiwa na kuongezeka kwa ushiriki wa vikundi vya uhalifu wa kupangwa.

Katika miaka michache iliyopita, vifaa zaidi vimeunganishwa na kudhibitiwa kwa kutumia mtandao. Kwa mfano, Kamera za CCTV, Magari, mifumo ya upachikaji wa maeneo kwenye ramani, runinga, na jokovu. Hii inaitwa teknolojia ya mtandao wa mambo [Internet of Things (IoT)]. Walakini, wataalam wa Usalama wa Mtandao wanaashiria tatizo kuwa ni kutolindwa vizuri kwa vifaa vya IoT. Kwa hivyo, vifaa hivi vya IoT visivyo salama vinatoa njia mpya, rahisi za kuiba habari za kibinafsi au kupata takwimu muhimu au mitandao. Kando na hayo, Wahalifu wa mtandao hutengeneza roboti za mtandao (botnets) ambazo zinaweza kuunda mashambulizi makubwa ya kukataza kufikia huduma kwenye mifumo inayowafanya wapatikane kwa watumiaji halali.

Mambo yafuatazo yanaendelea kukuza ukuaji wa gharama ya uhalifu wa kimtandao: Wahalifu wa mtandaoni wanakumbatia teknolojia mpya za mashambulizi, watumiaji wengi wapya wa mtandao wanatoka katika nchi zilizo na ulinzi dhaifu wa mtandao, uhalifu mkondoni unakuwa rahisi kupitia uhalifu wa mtandaoni na miradi mingine ya biashara. Wahalifu wa mtandaoni wanazidi kuwa na utata mwingi wa kifedha, na kuifanya iwe rahisi kupata mapato kutokana na matumizi yao na kwa kutumia mtandao bila kujulikana kupitia Tor na Bitcoin kama zana zinazopendwa kukuza vitendo vyao.

Kulingana na ripoti ya Novemba 2016 ya Tume ya Umoja wa Afrika [African Union Commission (AUC)] na kampuni ya usalama wa mtandao Symantec, kati ya nchi 54 barani Afrika, 30 zilikosa vifungu maalum vya kisheria vya kupambana na uhalifu wa kimtandao na kushughulikia ushahidi wa kielektroniki. Ufahamu mdogo wa umma na wakati mwingine ukosefu wa mifumo ya kisheria umezidisha tatizo.

Mashambulizi kutumia programu maalum (malware)pia yamekuwa tishio kwa takwimu inayoshikiliwa na serikali, biashara za ushirika, na za kibinafsi ikisababisha wizi, kufutwa, na usimbaji fiche wa habari.
Kwa kuwa imekuwa rahisi kufikia vifaa vya mawasiliano na pia vinaweza kupatikana kwa bei rahisi, uhalifu wa kimtandao umeonekana kuwa shida ya kawaida kwa umma na pia kwa watekelezaji wa sheria. Tayari, karibu uhalifu wote unaoripotiwa una kipengele cha uhalifu wa mtandaoni. Uhalifu kama vile ulaghai, biashara ya dawa za kulevya, magendo ya watu, kuenea kwa silaha ndogo ndogo, na uhalifu wa mazingira, vyote kwa mara nyingi vina sehemu hii kwani zitahusisha simu, kubadilishana barua pepe, ujumbe mfupi, matumizi ya majukwaa ya mitandao kama Facebook, Twitter, WhatsApp, uhifadhi wa habari; na kutuma pesa kupitia rununu kati ya nyengine.

Ijapokuwa uhalifu mwingi umekuwa wa utata/wa hali ya juu kwa sababu ya teknolojia, pia kwa njia fulani hutoa fursa kwa watekelezaji wa sheria kuchunguza kesi hizi kwa urahisi zaidi kwani kila wakati huwa kuna njia ya kufuatilia habari. Walakini, utekelezaji wa sheria unahitaji mafunzo yanayofaa na zana sahihi ili kuzuia, kugundua na kuchunguza kesi hizi kwa ufanisi. Maabara ya rununu na uchunguzi wa kutumia teknolojia na mifumo ya ulinzi wa mtandaoni ni muhimu katika suala hili.

EAPCCO imekuwa ikifanya kazi na UNODC kuunda Mwongozo wa Uchunguzi wa Uhalifu wa Mtandaoni.