Mafanikio

Tangu kuanzishwa kwake, EAPCCO imeendelea kusajili mafanikio makubwa katika hamu yake ya kufikia lengo lake la jumla la kukuza ushirikiano wa utekelezaji wa sheria za kikanda kama chombo cha kupambana na Uhalifu wa kupangwa wa Kimataifa.

  1. Uanachama: tangu kuanzishwa kwake, uanachama wa shirika umeongezeka mara mbili kutoka saba wakati wa kuanzishwa hadi kumi na nne kwa sasa. Huu ni ushuhuda ulio wazi kwamba maadili na maono ya EAPCCO yanavutia nchi zaidi ambazo zinaona kama ni shirika linalostahili katika usanifu wa usalama wa kikanda.
  2. Ushirikiano wa kikanda katika kupambana na uhalifu: Nchi katika kikanda hiki zinaendelea kushirikiana katika ngazi zote; za pande mbili na pande nyingi ili kupambana na Uhalifu wa kupangwa wa Kimataifa. Kusambaza habari, kusaidiana kisheria, na kukabidhi mhalifu kwa nchi inayopasa ni nguzo muhimu za ushirikiano wa kikanda katika kupambana na uhalifu.
  3. Shughuli za pamoja za Kikanda: Tangu 2010, Nchi ambazo ni Wanachama zimekuwa zikifanya operesheni za pamoja kulenga vikundi vya wahalifu wanaojipanga. Shughuli hizi mara nyingi zimepanuliwa zaidi ya Afrika Mashariki hadi mikanda mingine Afrika na kwingineko. Operesheni hizi hazijasaidia tu kukomesha uhalifu uliopangwa kwa kusambaratisha mashirika yaliyopo lakini pia zimeimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazoshiriki.
  4. Vituo vya Ubora vya Kikanda: Wazo la kuanzishwa kwa Vituo vya Ubora limekuwa ufanisi mkubwa wa shirika hili. Limekuwa mfano ndani ya dhana pacha ya mfano wa kuigwa na utendajikazi mzuri, Vituo vya Ubora vimeundwa ili vitumike kama taasisi bora katika kitengo chao kinachotoa huduma zao kwa kikanda chote. Karibu nchi zote zimejitolea kuwa na Kituo kimoja cha Ubora na angalau taasisi tatu kama hizo zinafanya kazi sasa. Hizi ni; Kituo cha Ubora juu ya amri ya Mwandamizi huko Musanze katika Jamhuri ya Rwanda, Maabara ya uchunguzi ya Kimaeneo huko Khartoum Jamhuri ya Sudan, na Kituo cha Ubora cha Kukabiliana na Ugaidi cha EAPCCO jijini Nairobi Kenya. Vituo vingine bado vinaendelea kutengenezwa.
  5.  Michezo ya kikanda: Hatua nyingine muhimu imekuwa katika nyanja ya michezo ambapo Baraza la Wakuu wa Polisi liliidhinisha kushiriki kwa maafisa wa polisi katika michezo ya kikanda kila mwaka. Shughuli ya kwanza ya michezo ya EAPCCO ilisimamiwa na Jamhuri ya Uganda mnamo 2017 na baadaye, hafla hizi zimekuwa zikiandaliwa na kutekelezwa kila mwaka. Kufikia sasa michezo hii imefanyika katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamuhuri ya Kenya. Hafla ya nne kama hiyo iliyopangwa kwa Jamuhuri ya Rwanda mnamo 2020, kwa bahati mbaya ilivurugwa na kuzuka kwa COVID 19. Michezo hii sio tu kutoa nafasi ya kushindana lakini pia kama njia ya kupumua- kwa watekelezaji wa sheria walio na shughuli nyingi ili kufanyisha zoezi miili na akili zao. Ushirikiano wa kikanda unakuzwa kama lengo kuu.
  6. Maazimio ya Wakuu wa Polisi: Tangu kuanzishwa kwake, wakuu wa polisi walitoa maazimio mengi juu ya ushirikiano wa polisi, kuoanisha sheria na sera na kusambaza habari.
  7.  Utengenezaji wa stakabadhi: Kwa msaada wa washirika, shirika limebuni stakabadhi kama vile miongozo ya Mafunzo na Taratibu za Uendeshaji ambazo ni muhimu katika kujenga uwezo wa utekelezaji wa sheria.
  8. Mafunzo ya Pamoja: Mipango ya mafunzo ya pamoja imeandaliwa na kufanyika katika nchi ambazo ni wanachama. Kwa jumla, zaidi ya maafisa 4,000 wa polisi wamepewa mafunzo tangu kuanzishwa. Hizi ni pamoja na shughuli za nyanjani, majadiliano kuhusu changamoto fulani, na shughuli za kuiga.
  9. Mkusanyiko wa Washirika: Kwa miaka mingi, shirika limepata na kudumisha washirika muhimu wa kimkakati ambao inafanya kazi nao kwa karibu kutekeleza lengo yake.
  10. Jarida la EAPCCO: Machapisho manne ya jarida hili la kuelimisha yamechapishwa. Jarida hili lina vifungu vinavyoangazia changamoto usalama wa kikanda na mikakati ya kuzishughulikia changamoto hizi na pia za zamani, za sasa na za baadaye.
  11. TOVUTI YA EAPCCO: Hili ni jukwaa la mawasiliano la hivi karibuni linalotoa fursa ya kuwajulisha na kushirikisha raia wa Afrika Mashariki na washirika wetu.