Biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya

Kwa miongo kadhaa, Pwani ya Afrika Mashariki imekuwa njia inayojulikana na inayopendelewa zaidi ya usafirishaji wa heroine kutoka maeneo ya uzalishaji huko Afghanistan na Pakistan. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi kadhaa zimeripoti kushika heroin nyingi, ambayo ni dalili ya shughuli zenye utata za washirika wanaohusika katika biashara hii haramu. Ijapo mara nyingi mihadarati hii huwa inasafirishwa kwenda kwenye masoko ya nje ya nchi, upatikanaji wa heroin kwa idadi ndogo kwa matumizi ya ndani ni dhahiri na umekithiri. Mbali na heroin, mihadarati mingine iliyo na mienendo mikubwa ya usafirishaji katika kikanda hiki ni bangi ambayo hukuzwa na kutumiwa sana katika eneo hilo na inachangia karibu 95% ya utumiaji haramu wa dawa za kulevya katika Afrika Mashariki; cocaine ambayo pia ilinaswa kwa idadi kubwa hapo zamani na crystal meth ambayo uzalishaji na usafirishaji wake umeongezeka na ni wasiwasi unaoibuka na unaipa Afrika Mashariki umaarufu kama njia mbadala ya usafirishaji wa cocaine, njia kuu ikiwa kupitia Afrika Magharibi. Kisha wasiwasi mwingine unaoibuka katika kikanda hiki ni kuongezeka kwa utumiaji wa Vitu vipya vya kisaikolojia na tishio la ulanguzi wa dawa za kulevya juu ya mtandao fiche.

Athari ambazo dawa hizi za kulevya zimekuwa nazo kwa idadi kubwa ya watu na hasa kwa vijana, ni mbaya sana.

Kwa kukabiliana na changamoto hii, nchi ambazo ni wanachama zimekuwa kivyao au chini ya mwavuli wa EAPCCO na INTERPOL zikifanya shughuli zinazolenga ulanguzi na biashara haramu ya dawa za kulevya. Operesheni kama vile USALAMA na LIONFISH MIHADARATI si kwamba tu zimesababisha kukamata kwa aina tofauti za dawa za kulevya, lakini pia zimesababisha kuimarishwa kwa kusambaza habari na ushirikiano kati ya nchi ambazo ni wanachama.

Drug-Trafficking

Baraza la Wakuu wa Polisi pia limekuwa muhimu katika kuzihimiza nchi kuoanisha sheria za dawa za kulevya ili kuboresha adhabu ya wakosaji.

Kuhusu kujenga uwezo, nchi ambazo ni wanachama zimepokea na zinaendelea kupata msaada kutoka kwa INTERPOL, EAC, na UNODC kando na washirika wengine.