KENYA KWENYE RADA YA FBI KWA SABABU YA UHALIFU WA MTANDAONI ULIOKITHIRI

Home/News/KENYA KWENYE RADA YA FBI KWA SABABU YA UHALIFU WA MTANDAONI ULIOKITHIRI

Kenya iko kwenye rada ya ofisi ya upelelezi ya shirikisho ya Marekani [US Federal Bureau of Investigation (FBI)] kama chanzo cha utapeli na kunakotumwa pesa zinazopatikana kutokana na wizi wa kifedha wa mtandaoni.

Repoti mpya ya Interpol iliyotolewa Agosti 14 kuhusu uhalifu wakupangwa wa mtandaoni Afrika ambayo ilionyesha jinsi kufanya mambo kidijitali kunawarahisishia wahalifu, na Interpol imeijumuisha Kenya kati ya nchi ambamo uhalifu wakupangwa wa kimataifa unatekelezwa.