Kikosi Cha Polisi Cha Ushelisheli
seychelles police

Kikosi cha polisi cha Ushelisheli kilianzishwa mnamo 1775. Askari 15 kutoka Mauritius waliletwa ili kutekeleza majukumu ya usalama. Mnamo 1802, kikosi cha polisi cha ndani kiliundwa chini ya amri ya Bw. Savy a Seychellois. Mnamo 1814, Ushelisheli ilijisalimisha kwa ukoloni wa waingereza na kwa miaka 100 iliyofuata, hakukupeanwa chochote kikubwa au chochote kabisa cha kudumisha sheria na nidhamu. Pengine hii ilikuwa ni kwa sababu hakukuwa na uhalifu katika muda huo na lengo la kitengo cha wanajeshi lilikuwa kupeana usalama wa nje na usalama wa ndani kwa kiwango cha chini.

Kuanzia 1840 mpaka 1875, rekodi haiwezi kupatikana kwa sababu mwaka wa 1862, kulikuwa na maporomoko ya ardhi yaliyoyaacha maeneo ya mji kuwa katika hali ya ukiwa na kituo cha polisi kilikuwa kwenye njia ya maporomoko hayo na rekodi zote zilipotea. Kutoka wakati huo mpaka 1879, ni vituo vichache tu vya polisi vilivyojengwa ikiwa ni pamoja na kimoja kilichokuwa Victoria. Nguvu kwa wakati hiyo ilikuwa ya wanaume 45.

Makao makuu ya polisi yaliyopo sasa yalijengwa 1950. Kulikuwa na mapikipiki 6, magari 2 aina ya land rover na land rover moja ya injini ya moto. Mwaka wa 1960, polisi walianza kujipanga tena. Kulikuwa na mkuu mpya wa polisi, mfumo mpya wa kuweka doria, nguvu ziliongezeka, vituo vingi vya polisi vilijengwa ikijumuisha Praslin na La Digue. Mwaka wa 1967. Polisi walikuwa wa kisasa zaidi, gari za kuweka doria zilianzishwa, mawasiliano ya radio yaliambatanisha vituo vyote vya polisi. Afisa wa Ushelisheli aliungwa mkono kwa ajili ya masomo maalum ya polisi wa Metropolitant na katika yadi mpya ya Uskoti huko London, kuanzisha na matumizi ya alama za vidole, kuundwa kwa shirika la uchunguzi wa upigaji picha na maeneo ya uhalifu. Kikosi spesheli kilichokuwa na wanaume 45 pia kiliundwa ili kukinga machafuko ya raia, kusaidia majukumu ya jumla inapohitajika. Mwaka wa 1968, wanawake 6 walihitajika kuwa kama maafisa wa polisi. Kabla hapo, walikuwa konstebo maalum tu.

Mwaka wa 1974, shule mpya ya mafunzo ilifunguliwa katika kisiwa cha Praslin kikiwa na nafasi ya kutosha wanafunzi 40 wa kulala hapo. Hii ilileta kozi bora zaidi katika sheria na utaratibu, kozi za usimamizi kwa Sajenti na Inspekta zilianzishwa, kuongezwa kwa idadi ya maafisa wa ngazi za juu kwenda kwa mafunzo ng’ambo. Kikosi kiliendelea kuboreka kupitia ushawishi wa Uingereza. Washelisheli walikuwa wanajimudu kisiasa na uhitaji wa kuwa wa kisasa na kujipanga tena kwa polisi.

Mnamo 1993, Ushelisheli ilibadilika kutoka kuwa serikali ya chama kimoja hadi mfumo wa demokrasia. Ilikuja na uanzilishi wa katiba mpya. Kuanzishwa kwa kikosi cha polisi kumehakikishwa chini ya kifungu 159 (1) cha katiba ya Jamhuri ya Ushelisheli. Kifungu cha 159 (2) kinataja sheria ya kukipanga na kukisimamia kikosi cha polisi, ambayo ni ‘Sheria ya kikosi cha polisi’. Kifungu cha 160 (1) kilitaja uteuaji wa Kamishna wa Polisi kuendesha kikosi cha Polisi.

Kazi ya polisi.
Kifungu cha 161 cha katiba sehemu ya 6 cha sheria ya kikosi cha polisi kinataja kazi ya kikosi cha polisi kwa ujumla.
• Kudumisha sheria na nidhamu
• Kuzuia na kutambua uhalifu Ushelisheli
• Kudumisha amani ya umma
• Kukamatwa kwa wahalifu
• Kufanya majukumu mengine kama yanavyoelezwa na sheria.

Kamishna wa polisi anateuliwa na raisi, na inategemea kupitishwa na bunge la taifa. Ana amrisha, simamia, elekeza na kudhibiti kikosi cha polisi

Kamishna wa sasa ni Bw. Ted Barbe.

Dhamira
Kuzuia chochote kinachoweza kuwa tishio kwa usalama au ulinzi wa jamii yoyote; Kuchunguza uhalifu wowote unaotishia usalama na ulinzi wa jamii yoyote; Kuhakikisha wahalifu wanafikiswa mahakamani; na Kushiriki katika shughuli za kushughulikia chanzo cha uhalifu.
Maono
Kutengeneza mazingira salama na salama kwa watu wote
Mahitaji ya kujiunga
Kuonyesha tabia nzuri katika jamii
Umri wa kati ya miaka 18 na 30 wakati wa uteuzi wa kwanza
Kuwa kwa hali ya sawa kimatibabu na kimwili
Mwenye kimo cha sawa
Kufuzu vyema kimasomo na kupita mtihani wa kujiunga. Maafisa wa polisi wana uwezo wa kuendelea katika madaraja ya Konstebo anayefunzwa, Konstebo, Koplo, Sajenti, Inspekta mdogo, Inspekta, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Mrakibu, Mrakibu Mkuu, Naibu Kamishna wa Polisi hadi Kamishna wa Polisi.