Huduma Ya Kitaifa Ya Polisi Ya Sudan Kusini
ssudani

Nchi: Jamhuri ya Sudan Kusini
Jina la shirika: Huduma ya Kitaifa ya Polisi ya Sudan Kusini [South Sudan National Police Service (SSNPS)]
IGP wa sasa: Generali Majak Akec Malok
Anwani: Wizara ya mambo ya ndani/RSS, S. L. Posta 600
Akaunti ya facebook: South Sudan National Police Service

Usuli kwa ufupi wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi ya Sudan Kusini
Mabadiliko ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi ya Sudan Kusini [South Sudan National Police Service (SSNPS)] yalifanyika katika zama za ukoloni hapo mwaka wa 1820 na 1898 uliokuwa wakati wa waMisri-Turko na waMisri Anglo mtawalia, ambapo kila utawala wa ukoloni walianzisha kikosi cha polisi kulinda utawala wao wa kiukoloni. Baada ya uhuru wa Sudan hapo 1956, kikosi cha polisi cha Sudan kilikuwa kiko katika mikoa yote ikiwa ni pamoja na mikoa ya Sudan.

Wakati wa mapambano ya ukombozi, kikosi cha wanajeshi/wanaharakati wa watu wa

Sudan [Sudan People’s Liberation Army/Movement (SPLA/M)] kilianzisha kikosi cha polisi hapo 1994 ili kuleta huduma ya polisi katika maeneo ya Sudan Kusini yaliyokombolewa ya SPLA. Hii iliendelea mpaka wakati wa Mkataba wa Amani Kamili [Comprehensive Peace Agreement (CPA)] mwaka wa 2005 ambapo Sudan Kusini ilipewa utawala wa uhuru, na ikasababisha kuanzishwa kwa Huduma ya Polisi ya Sudan Kusini [South Sudan National Police Service (SSPS)].

Baada ya uhuru wa Jamhuri ya Sudan Kusini tarehe 9 Julai 2011, Huduma ya Polisi ya Sudan Kusini [South Sudan Police Service (SSPS)] ilibadilishwa jina ikaitwa Huduma ya Kitaifa ya Polisi ya Sudan Kusini [South Sudan National Police Service (SSNPS)] na wanachama wa SPLA (Wanajeshi wa ukombozi wa watu wa Sudan [Sudan People’s Liberation Army]) na kikosi cha polisi cha Sudan viliunganishwa na likapewa jukumu la kimsingi la kuzuia, kutambua na kuchunguza uhalifu, kudumisha sheria na nidhamu, kuwalinda watu na mali zao na kusimamia na kutekeleza katiba na utawala wa sheria.

 

 

 

 

IGP Gen. Majak Akec Malok

 

 

 

Head of INTERPOL NCB JUBA Maj. Gen. Amou Anyieth Reec

Ministry of Interior